Fighting Malaria
|
Published in April 2007 | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Je, wafanya kazi gani ? Mimi ni mke wa nyumbani. Global Fund nimeisikia. Walipita masheha wakawa wanaandika watoto wote ambao hawajafika miaka mitano. Halafu ikatoka tangazo kwenye redio kwamba neti zitatoka, na sehemu. Ilipofika siku tulichukuwa neti. Sio mbali sana kwa sababu ilitafutwa senta hapa kwetu. Sijui utaratibu uliotumika. Na umefurahishwa na matokeo ? Naam, kwa sababu mtoto amepata chandarua cha bure, ni kama zawadi yake. Saa hizi ana miaka sita.
Labda nizungumzie kwa familia ya kwangu. Kwa sababu familia nyengine sitoweza kuijua. Yangu imekuwa ni afadhali, kwa sababu naangalia ule mda mtoto ameenda hospitali. Nikichukulia ameenda hospitali mwezi wa nne wa mwaka jana, na amerudi tena hospitali Februari ya mwaka huu 2007. Na pia siyo kama amerudi hospitali kwamba ana malaria; alipoangaliwa , ni ‘negative’ malaria, isipokuwa tu anasumbuliwa na pumzi. Ni mafanikio. Kabla ya kupata chandaruwa, alikuwa akienda hospitali mara ngapi? Alikuwa akienda mara mbili au tatu kwa mwaka. Dawa za malaria, tulikuwa ukienda kituoni hamna. Tunaenda kununua zetu binafsi, lakini kwa wakati huu tunaona kama dawa zinapatikana. Sasa hivi, hiyo pesa unaitumiaje - na unayo mengine ya kusema? Siku hizi naitumia pesa kununua malishi bora ya mtoto. Sina chochote- isipokuwa jamii tu- ielewe kwamba ni nini malaria, vipi unapata malaria- kisha watajua namna gani ya kujikinga na malaria. |
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||



Sasa, ungeweza kuniambia, maisha ya familia yako ama ya jamii imebadilikaje ?